LIVE UPDATES: Matokeo ya Uchaguzi Mkuu Tanzania 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, October 26, 2015

LIVE UPDATES: Matokeo ya Uchaguzi Mkuu Tanzania 2015.

MAPUNDA
Sixtus Mapunda.

Mbiga Mjini: Mgombea Sixtus Mapunda (CCM), ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa ubunge katika Jimbo la Mbinga Mjini akipata kura 28,324.

ESTER MATIKU
Ester Matiku.

Jimbo la Kahama Mjini: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba (CCM), ametangazwa kuwa mshindi wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana October 24,2015.

Jimbo la Monduli: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli (CHADEMA), Julius Kalenga ametangazwa kuwa mbunge wa jimbo hlio.

Jimbo la Nzega Mjini: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM) ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa jimbo hilo.

Jimbo la Ilemela: Mgombea Ubunge Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula (CCM) ametangazwa rasmi mshindi wa jimbo hilo kwa kumbwaga mpinzani wake aliyekuwa mbunge ya jimbo hilo, Highness Kiwia (Chadema). Tarifa zaidi zinasema Kiwia hakuwepo wakati wa kutangazwa matokeo hayo.

Jimbo la Moshi Mjini: Mgombea Ubunge Jimbo la Moshi Mjini, Japhary Raphael Michael (CHADEMA) ametangazwa rasmi mshindi wa jimbo hilo kwa kupata jumla ya kura 51656 na kumuangusha Davis Mosha wa CCM.

Jimbo la Bunda Mjini: Mgombea Ubunge Jimbo la Bunda Mjini, Ester Bulaya (CHADEMA) ametangazwa rasmi mshindi wa jimbo hilo na kumuangusha Steven Wasira.

Jimbo la Siha: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Siha kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA, Dk. Godwin Mollel,ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa jimbo hilo.

Arumeru Mashariki: Joshua Nassari wa Chadema ameshinda ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki akipata kura 86694.

Tarime Mjini: Ester Matiku wa Chadema ameshinda ubunge Jimbo la Tarime Mjini akipata kura 20,017, Michael Kembati CCM akipata kura 14,025 na Deogratius wa ACT kura 336.

Lindi Mjini: Hassan Suleiman Kaunje (CCM) ametangazwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Manispaa ya Lindi, kuwa Mbunge Mteule wa Jimbo la Lindi Mjini.

Mbinga Vijijini: Mgombea Martin Msuha (CCM) ametangazwa rasmi na Msimamizi wa Uchaguzi, Venance Mwamengo kuwa mshindi wa ubunge katika Jimbo la Mbinga Vijijini baada ya kupata kura 59,269.

Tunduma: Mgombea Mwakajoka Frank (Chadema) ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa ubunge katika Jimbo la Tunduma (Mbeya) akipata kura 32,442. Matokeo hayo yametangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi Halima Mpita.

Tandahimba: Mgombea Ubunge wa CUF katika Jimbo la Tandahimba mkoani Mtwara, Ahmed Katani ametangazwa kuwa mshindi wa jimbo hilo.

Musoma Mjini:  Mgombea Vedatus Mathayo (CCM) ametangazwa rasmi na Msimamizi wa Uchaguzi kuwa mshindi wa ubunge katika Jimbo la Musoma Mjini baada ya kupata kura 32,836.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad